Emmanuel Msoma Shija
Wasifu:
Emmanuel alizaliwa tarehe 3 April 1987. Alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya catering ya FANINA. Alikuwa ni dereva. Alipenda sana gym. Ameacha mke na watoto wawili.
Alipoonekana mwisho: Dar es Salaam
Alikuwa nyumbani tu, akatoka maramoja na akapigwa risasi tarehe 29 Oktoba 2025 na polisi waliopita doria manyumbani na defender wakipiga risasi kiholela. Alipigwa kwenye ini akapoteza damu na kufariki. Mkewe (Veronic Lyimo)ameongea na vyombo vya habari kuelezea jinsi daktari walivoripoti tofauti kwenye cheti cha kifo kuwa alikuwa ana shida ya uti wa mgongo. Mkewe asimulia kuwa walipata mwili siku ya 6, mwili ukiwa umeshaoza nakutoa harufu; walimzika Kinondoni.